Wazee wa Jamii ya Tiriki Waitaka NEMA Kuwashirikisha Katika Utunzi wa Mazingira

0
120
Photo credit: https://guardian.ng/saturday-magazine/cover/edo-forest-reserves-depleted-in-lull/

 

Mamlaka ya utunzi wa mazingira – NEMA imetakiwa kuwashirikisha kikamilifu wazee wa jamii ya Tiriki katika utunzi wa mazingira ya misitu yao.

Wakiongozwa na Simeon Andashe,  wazee wa jamii ya Tiriki wilayani Hamisi kaunti ya Vihiga wanasema kutohusishwa kwao katika utunzi wa mazingira kumechangia kuharibiwa kwa misitu hiyo.

Andashe anasema hali hii imechangia misitu hiyo kuharibiwa huku miti ikikatwa kiholela kwa matumizi ya kuni.

Aidha, ameilaumu mamlaka hiyo akisema, uongozi wa sasa haushirikiani nao kufahamisha jamii umuhimu wa utunzi wa mazingira.

”Tangu kabadilishwa kwa usimamizi wa NEMA wa awali kaunti ya Vihiga, tumeachwa nje ya maswala ya utunzi wa mazingira ya misitu hii,” akasema Andashe.

Andashe amesisitiza kuwa ushirikiano kati yao na mamlaka ya utunzi wa mazingira utachangia pakubwa kuokoa misitu hiyo anayosema ina manufaa mengi zaidi huku ikitegemewa kwa dawa za kienyeji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here